Mkasi | SO9E13 With Wagosi Wa Kaya Extended Version
Uploader: MkasiTV
Original upload date: Tue, 16 Sep 2014 00:00:00 GMT
Archive date: Sat, 04 Dec 2021 01:31:27 GMT
Tasnia ya Muziki Tanzania ilipata sura mpya na mtazamo mpya tangu kipindi cha miaka ya 2000 pale tulipoona watu kama Mr. Ebbo, Professa Jay, Juma Nature, Daz Nundaz na wengineo wakianza kuimba nyimbo
Show more...
zenye Mrengo wa kiharakati zaidi na kukubalika za jamii kwa upana zaidi. Lakini hakuna waliotikisa anga za muziki kwa nyimbo zenye Ujumbe mzito na Ushawishi wa Kiwanaharakati na kisiasa kama hawa Wawili, nao ni John Evans Simba (Dakta John) na Fredrick Gerson Mariki (Mkoloni) au kama wengi tunavyowafahamu kama WAGOSI WA KAYA.
Kwanza kabisa, Wagosi Wa Kaya walianza kwa kubadili aina ya Ujumbe uliokuwa unapatikana kwenye muziki wa kizazi kipya, kwa kuongelea mambo ya kila siku yanayosumbua jamii bila kuweka kificho cha aina yoyote. Pili ni aina ya lugha na lafudhi waliyotumia, ambapo matumizi ya Lafudhi ya Kidigo na Kisambaa. Hilo na kuchanganya na lugha ya ucheshi ya kufikisha ujumbe, vilimfanya msikilizaji kuupokea ujumbe ilihali akiwa anaburudika.
Dkt John na Mkoloni wana historia ndefu na Tanga, John alikulia akikata Mashamba ya Mkonge na kupata elimu ya msingi ilihali akiendelea kupambana na changamoto za kimaisha katika familia yao. Alishawahi kunukuliwa akisema kuwa aliwahi kufanya kazi kwa kukodishwa, yaani wanachukuliwa na mtu kwenda kufanya kazi kwenye mashamba, na hatimae aliewapeleka alilipwa na yeye kuwalipa vibarua ujira wao huku akibaki na sehemu ingine kama faida yake. Kwa upande wa Mkoloni, ingawa sehemu kubwa ya familia yake, hasa wazazi wakiwa Jijini, yeye alikulia Tanga ambako jamii yao ilikua ina tawi pia. Elimu pia alipatia mkoani Tanga katika shule ya Popatlal.
Kuingia katika sanaa, Kuibuka kwa kundi hili katika sanaa za muziki kulianza na mapenzi ya dhati waliyokuwa nayo kwenye fani. John alianza kama Densa na mara nyingi alijiweka katikati ya shughuli na kutoa burudani kutipia ufundi wake wa “Kubreak Dance”. Ni Baada ya kukutana na Fredrick aliekuwa na kundi la Tanga Line, na wengi mtamkumbuka Dani Msimamo ambae pia ni mmoja kati ya vinara wa kundi hilo. Baada ya hao wawili kubadilisha mistari iliyokuja kuzaa tungo ya “TANGA KUNANI” ndipo wakaona ipo haja ya kutoka kama kundi na kufanya kazi pamoja kama Wagosi wa Kaya. Kuibuka kwa kundi hili sio tu kulisaidia kuiweka Tanga katika Ramani ya Muziki wa Tanzania na Afrika Mashariki, lakini pia kulisiaidia kwa kiasi kikubwa kuibua ukweli juu ya Mji huu Mkongwe ambao hapo awali uliwahi kuvuma kama Kitovu cha Biashara, Kilimo, Viwanda na Uchukuzi.
Katika kipindi chao kama kundi, Wagosi walipata mafanikio makubwa sana wakiwan chini ya muandaaji muziki Profesa Ludigo na Studio za MJ, na moja kati ya vibao vilivyowapa umaarufu sana ni pamoja na TANGA KUNANI, WAUGUZI, TRAFIKI. Hivi karibuni baada ya kupotea kwa muda, wamejiunga tena na kurudi wakiwa wanaandaa tungo kadhaa za kuwarejesha tena kwenye ramani. Ingawa wanakiri kuwa kurejea baada ya kuwa nje ya “game” kwa muda mrefu ni kazi, kwani kuna wale waliokuwepo nao wakaendelea kuwepo, na kuna wengi wapya walioibuka kwa kasi ya juu na bado wapo juu. Mnamo April mwaka 2014 waliachia Video mbili mpya za nyimbo za “Bao” na “Gahawa”, na wanaahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii kuendelea kuwaburudisha mashabiki wao wa zamani na wapya.
Katika Mkasi TV, tulipata fursa ya kuzungumza nao, Salama, Mubarak na John waliweza kuhoji mengi zaidi. Sikia na kutazama toleo hili kamili la video hapa hapa.
FURAHIA
L . O . V . E
Follow MkasiTV on
Facebook : http://facebook.com/MkasiTV
Twitter : @MkasiTV